Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa amali za maiti hukatika kwa kufa kwake, hayapatikani mema tena baada ya kifo chake isipokuwa kwa mambo haya matatu; kwa sababu yeye ndiye aliyekuwa sababu ya kupatikana kwake: La kwanza: Sadaka yenye kuendelea thawabu zake na kudumu, isiyokatika, kama wakfu, na kujenga msikiti, na kuchimba visima, na mengineyo. La pili: Elimu wanayonufaika nayo watu, kama kutunga vitabu vya kielimu, au kama kumfundisha mtu, yule naye akaisambaza elimu hiyo baada ya kifo chake. La tatu: Mtoto mwema muumini wa kumuombea dua mzazi wake.