Mtume rehema na amani ziwe juu yake alikuwa mkarimu zaidi kuliko watu wote katika mwezi wa Ramadhani, kiasi ambacho alikuwa akitoa kinachostahiki kumpa anayestahiki, na sababu ya kuzidisha ukarimu huu ni mambo mawili: La kwanza: Ni kukutana kwake na Jibril amani iwe juu yake. Na jambo jingine: Ni kuirejea Qur'ani, nayo ni kuisoma pasina kutazama mahali ilipoandikwa. Kwa hiyo Jibril, amani iwe juu yake, alisoma naye kila kilichoteremshwa katika Qur'ani, na Mtume wa Mwenyezi Mungu rehema na amani ziwe juu yake ni mkarimu zaidi, na ni mtenda kheri zaidi, na ni mwepesi wa kunufaisha viumbe kuliko upepo mzuri anaoutuma Mwenyezi Mungu kwa ajili ya mvua na rehema.