Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakwamba mtu aliyekamilika zaidi kiimani ni yule itakayekuwa nzuri tabia yake, na hii kwa kuwa na uso mkunjufu, na kutenda mema, na maneno mazuri, na kuacha maudhi. Na muumini bora kuliko wote ni yule mbora kwa wake zake, kama mke wake na mabinti zake na dada zake na ndugu zake wengine wa kike; kwa sababu wao ndio watu wenye haki zaidi kutendewa tabia nzuri.