Anaeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba Mwenyezi Mungu amewajibisha mambo na akafaradhisha faradhi basi shikamaneni nazo na wala msifanye uzembe katika hayo kwa kuyaacha au kuzembea ndani yake, na akakuwekeeni vizuizi na makemeo yaliyokadiriwa yanayokuzuieni na kukukemeeni katika yale asiyoyaridhia, msizidishe zaidi ya yale yaliyoamrishwa na sheria, na akaharamisha maharamisho kadhaa msiyachukue na wala msiyakaribie, na yasiyokuwa hayo kayaacha na akayanyamazia kwa kuwahurumia waja wake, hivyo yanabakia katika asili ya uhalali wake basi msiyatafute.