Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa yeyote atakayefanya dhambi zinazohitaji adhabu ya kisheria, kama vile uzinzi au wizi, na akapata adhabu hiyo na ikatekelezwa duniani, basi adhabu hiyo itamfutia dhambi hiyo na kumuondolea adhabu ya Akhera. Hii ni kwa sababu Allah ni mkarimu na mwenye rehema, na hawezi kumuhukumu mja wake kwa adhabu moja mara mbili. Na ikiwa Allah amemsitiri mja wake duniani na hakumuhukumu kwa dhambi hiyo, na akamsamehe na kumghufiria, basi Allah Mtukufu ni mkarimu na mbora zaidi hawezi kurudi katika adhabu ya dhambi aliyoisamehe na kuifuta."