Anaeleza bin Abbasi radhi za Allah ziwe juu yao yeye na baba yake yakuwa alikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake siku ya kuchinja (Siku ya Idd kubwa) asubuhi ya kurusha vijiwe (kwa walioko Makka katika ibada ya Hija) katika Hija ya kuaga, Akamuamrisha amuokotee vijiwe vya kurusha, akamuokotea vijiwe saba, kimoja miongoni mwake kina saizi ya kijiwe cha kuwindia, akaviweka Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- mkononi mwake kisha akavitikisa, na akasema: Kwa vijiwe vya mfano kama huu basi rusheni, Kisha akatahadharisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kutokuchupa mipaka na kujilazimisha na kuvuka kiasi katika mambo ya dini, kwani kilichowaangamiza umma waliotangulia ni kuvuka mipaka na kujiwekea mkazo katika dini.