explain-icon

Ufafanuzi

Nikuwa Mtume rehema na Amani ziwe juu yake - Aliulizwa kuhusu kumtibu aliyerogwa kwa njia ambayo walikuwa wakiijua tangu zama za ujinga, mfano: kuondoa uchawi kwa uchawi ni ipi hukumu ya hilo, akajibu rehema na Amani zimfikie kuwa hiyo ni katika kazi za shetani, au hufanyika kupitia yeye; kwasababu inakuwa kwa aina ya uchawi na kwa kuwatumia mashetani, hiyo ni ushirikina na ni haramu. na ama kutibu uchawi kunakofaa: ni kuufungua uchawi kwa kisomo cha ruqya au kuutafuta, na kuufungua kwa mkono pamoja na kusoma Qur'ani au kwa dawa za halali.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Sheria ya kuwauliza wanachuoni katika yale yanayotatiza hukumu yake; kwa tahadhari ya kutoangukia katika haramu.
  • Katazo la kutibu uchawi kwa namna wanayoifahamu watu wa zama za ujinga; kwasababu ni uchawi na uchawi ni ukafiri.
  • Nikuwa kazi za shetani zote zimeharamishwa.