explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayeapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu na majina yake na sifa zake basi atakuwa kamkufuru Mwenyezi Mungu au kafanya ushirikina; kwa sababu kiapo humaanisha kutukuzwa mwenye kuapiwa, na utukufu ni wa Allah pekee; hakuapiwi ila kwa Allah na majina yake na sifa zake kutakasika machafu ni kwake. Na kiapo hiki ni katika shirki ndogo; lakini ikiwa muapaji atakitukuza alichokiapia kama anavyomtukuza Allah Mtukufu au zaidi; basi hapo itakuwa katika ushirikina mkubwa.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Nikuwa kutukuza kwa kiapo ni katika haki za Mwenyezi Mungu -Aliyetakasika na kutukuka- hakuapiwi ila kwa Allah na majina yake na sifa zake.
  • Pupa ya Masahaba katika kuamrisha mema na kukataza maovu, hasa hasa uovu unapokuwa unahusiana na ushirikina mkubwa au kufuru.