explain-icon

Ufafanuzi

Anasimulia Abuu Said Al-Khudri Mwenyezi Mungu amuwie radhi, kuwa alikuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake na haya zaidi kuliko msichana bikira ambaye hajaolewa na kuishi na wanaume aliyefichwa nyumbani kwake, na kwa sababu ya ukubwa wa aibu yake anapokichukia kitu uso wake unabadilika na wala hazungumzi, bali masahaba wake wanalibaini hilo katika uso wake.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kumebainishwa miongoni mwa sifa alizokuwa nazo Mtume rehema na amani zimshukie kama haya, ambayo ni tabia tukufu.
  • Haya ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake, maadamu hayajatendeka makatazo ya Mwenyezi Mungu, yakitendeka basi rehema na amani ziwe juu yake alikuwa akikasirika na kuwaamrisha maswahaba zake na kuwakataza.
  • Himizo la kujipamba na sifa ya haya; kwa sababu huisukuma nafsi kufanya mazuri na kuacha machafu.
explain-icon

Aina tofauti

explain-icon

Ziada