Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba kulikuwa na Mfalme mmoja katika umma zilizopita kabla yetu, na alikuwa na mchawi wake, alipozeeka mchawi, akasema kumwambia Mfalme: Bila shaka mimi nimezeeka, nitumie kijana ili nifundishe uchawi. Basi Mfalme akamtumia kijana ili amfundishe, kukawa katika njia ya kijana anapokwenda kwa mchawi kuna mchamungu, siku moja akakaa kwake na akasikiliza mazungumzo yake, yakampendeza, basi akawa kila anapokwenda kwa mchawi anapita kwa mchamungu anakaa kwake, anapofika kwa mchawi mchawi anampiga kwa sababu ya kuchelewa, akamlalamikia mchamungu kitendo hicho, akasema: Ukimhofia mchawi, basi mwambie: Nyumbani walinichelewesha, na ukihofia watu wako basi waambie: Mchawi alinichelewesha, basi wakati akiendelea kuisha katika maisha hayo, ghafla alifika mahali kulikuwa na mnyama mkubwa sana, aliyekuwa kawazuia watu kuendelea na shughuli zao, akasema: Leo ndio nitajua je, mchawi ndio bora au mchamungu ndio bora? Akachukua jiwe, akasema: Ewe Mwenyezi Mungu ikiwa suala la mchamungu linapendeka zaidi kwako kuliko jambo la mchawi basi muuwe mnyama huyu, ili watu waendelee na shughuli zao, akamrushia akamuua, na watu wakaendelea na shughuli zao, akamuendea mchamungu akamueleza, mchamungu akasema: Ee mwanangu wewe leo umekuwa bora kuliko mimi, jambo lako limefikia hapa ninapopaona, na kwa hakika utapewa mitihani, ikitokea umepewa mithani basi usimuoneyshe yeyote hapa nilipo, na wakati huo kijana alikuwa akiponya vipofu na wenye mbaranga, na akiwatibu watu kutokana na maradhi yote kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, akasikia taarifa hizi mmoja kati ya jamaa wa Mfalme alikuwa amekwishapofuka, akamuendea akiwa na zawadi nyingi, akasema kumwambia kijana: Zote hizi zilizoko hapa katika zawadi ni kwa ajili yako endapo utaniponya. Akasema: Hakika mimi simponyi yeyote, bali anayeponya ni Mwenyezi Mungu, ikiwa wewe utamuamini Mwenyezi Mungu nitakuombea na atakuponya, basi akamuamini Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu akamponya, akamuendea Mfalme, akakaa karibu naye kama alivyokuwa akikaa awali, Mfalme akasema kumwambia: Ni nani aliyekururejeshea macho yako? Akasema: Ni Mola wangu Mlezi, akasema: Hivi una mola mwingine zaidi yangu? Akasema: Mola wangu Mlezi na Mola wako ni Mwenyezi Mungu. Akamchukua na kumtesa, akaendelea kumpa mateso mpaka akamuelekeza kwa yule kijana, akaletwa yule kijana, Mfalme akasema kumwambia: Ee mwanangu, hivi uchawi wako ndio umefikia kiwango cha kuponya vipofu na wenye mbaranga, na unafanya kadhaa wa kadhaa. Akasema: Hakika mimi simponyi yeyote, bali anayeponya ni Mwenyezi Mungu, basi akamchukua akaanza kumtesa, akaendelea kumpa mateso mpaka akamuelekeza kwa yule mchamungu. Akaletwa yule mchamungu, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, akaagiza uletwe msumeno, akautia msumeno kati kati ya utosi wake, akamchana kwa msumeno huo vipande viwili. Kisha akaletwa yule jamaa wa Mfalme, akaambiwa: Rudi katika dini yako, akakataa, akautia msumeno kati kati ya utosi wake, akamchana kwa msumeno huo vipande viwili. Kisha akaletwa yule kijana, akaambiwa, rudi katika dini yako, akakataa, akamkabidhi kwa wanaume katika jamaa zake, walikuwa kati ya watatu mpaka kumi. Akasema: Nendeni naye mpaka katika mlima kadhaa wa kadhaa, kisha mpandisheni juu ya mlima, mkifikia kileleni, muulizeni, yuko tayari kurudi katika dini yake?, ikiwa atakuwa tayari kurudi basi muacheni, na asipokuwa tayari mtupeni chini, basi wakaenda naye na wakapanda naye juu ya mlima. Akasema yule kijana: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze dhidi yao kwa chochote ukitakacho, basi mlima ukawatetemesha, na ukatikisika mtikisiko mkubwa sana mpaka wakaanguka wote, na akarudi kwa Mfalme akiwa anatembea. Mfalme akasema kumwambia kwa mshangao mkubwa: Jamaa zako wamefanya nini?!! Akasema: Mwenyezi Mungu kanitosheleza dhidi yao. Basi akamkabidhi kwa kundi jingine katika jamaa zake, akasema: Nendeni naye mkambebe katika boti ndogo, kisha nendeni naye mpaka kati kati ya bahari, ikiwa atakuwa tayari kurudi katika dini yake basi muacheni, akikataa basi mtupeni baharini. Basi wakaondoka naye, akasema: Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze dhidi yao kwa chochote ukitakacho, basi boti ikawapindua wakawa wameangamia wote, na akarudi kwa Mfalme akiwa anatembea. Mfalme akasema: Wamefanya nini jamaa zako?!! Akasema: Mwenyezi Mungu kanitosheleza dhidi yao, kisha akasema kumwambia Mfalme: Hakika wewe huwezi kuniua mpaka ufanye nitakayokuamrisha. Akasema: Ni yapi hayo? Akasema: Uwakusanye watu katika uwanja wa wazi, na unitundike juu ya shina la mti, kisha chukua mshale mmoja kutoka katika ala yangu ya mishale, kisha weka mshale katikati ya upinde, kisha sema: Bismillaah -kwa jina la Mwenyezi Mungu- Mola wa kijana huyu, kisha nirushie, basi ukifanya hivyo bila shaka utaniua, basi akawakusanya watu katika sehemu mmoja, kisha akamtundika juu ya shina la mti, kisha akachukua mshale mmoja katika ala yake, kisha akauweka mshale kati kati ya upinde, kisha akasema: Bismillah -kwa jina la Mwenyezi Mungu- Mola wa kijana huyu, kisha akamrushia, mshale ukamchoma kati ya sikio lake na jicho lake, akaweka mkono wake mahala alipochomwa mshale, na akawa amefariki. Watu wakasema: Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu, Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu, Tumemuamini Mola Mlezi wa kijana huyu. Watu wakamfuata Mfalme wakamwambia: Unaona sasa, ulichokuwa ukikihofia? Bila shaka tunamuapa Mwenyezi Mungu kimekutokea ulichokuwa ukikihofia, ambacho ni watu kumfuata kijana huyo, na wote kumuamini Mola wake, akaamrisha Ardhi ipasuliwe mashimo makubwa ya msitatili (pembe nne) kati kati ya njia, na akawasha na kuuchochea moto ndani yake, na akasema: Yeyote ambaye hatorudi katika dini yake basi mtupeni humo, basi wakafanya alichokiamrisha Mfalme, mpaka akaja mwanamke mmoja akiwa na mwanaye mchanga, akasimama, na akabakia hapo na akachukia kuingia katika moto, basi mwanaye akasema kumwambia: Ewe mama yangu vumilia, kwani hakika wewe uko katika haki.