Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliomba dua ya udhalili na fedheha mpaka akahisi kana kwamba mtu ametia pua yake kwenye mchanga – akarudia mara tatu – akaulizwa: Ni nani huyo ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, uliyemuombea dua mbaya? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Atakayewakuta wazazi wake wawili, mmoja wao au wote wawili, wakati wa utuuzima, wakawa si sababu ya yeye kuingia Peponi; na hii ni kutokana na kukosa kuwatendea wema na kutowatii.