explain-icon

Ufafanuzi

Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakayekula au kunywa kwa kusahau akiwa kafunga swaumu ya faradhi au sunna basi atimize swaumu yake wala asifungue; kwa sababu hakukusudia kufungua, bali hiyo ni riziki Mwenyezi Mungu kamsogezea na akamlisha na kumnywesha.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kukubalika kwa swaumu ya aliyekula au kunywa kwa kusahau.
  • Hana dhambi aliyesahau akala au kunywa; kwa sababu hilo si kwa maamuzi yake.
  • Upole wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake na kuwafanyia wepesi juu yao na kuwaondolea tabu na uzito juu yao.
  • Hafungui mfungaji kwa chochote katika vile vyenye kufunguza ila zikikamilika sharti tatu: Ya kwanza: Awe anajua, akiwa mjinga hafungui, ya pili: Awe na kumbukumbu, kama kasahau swaumu yake ni sahihi na wala halazimiki kulipa, ya tatu: Iwe kwa hiari yake, na si kwa kulazimishwa, yaani atumie vyenye kufunguza kwa hiari yake mwenyewe.
explain-icon

Ziada