Alikataza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwapiga wanawake, akaja kiongozi wa Waumini Omari bin Khattwabi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wanawake wamepata ujasiri kwa waume zao, na wamekuwa na tabia mbovu. Akaruhusu rehema na amani ziwe juu yake kuwapiga kipigo kisichojeruhi inapopatikana sababu ya hilo, kama kukataa kwao kutimiza wajibu wao kwa waume zao na kuwaasi, na mfano wa hayo. Baada ya hapo wakaja wanawake kwa wake wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake wakishitakia kupigwa na waume zao kipigo chenye kujeruhi, na matumizi mabaya ya ruhusa hii, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Wanaume hao, wanaowapiga wake zao kipigo chenye kujeruhi, si watu bora kwenu.