Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ikiwa mwenye kuswali atasita katika swala yake na akashindwa kujua ameswali rakaa ngapi, tatu au nne? Hebu aondoe idadi iliyozidi yenye shaka na asiihesabu; tatu ndiyo ana uhakika nazo, basi ataswali rakaa ya nne, kisha atasujudu sijida mbili kabla ya kutoa salamu. Ikiwa aliswali nne kweli; basi zitakuwa tano kwa kuongeza rakaa moja, na sijida mbili za kusahau zitakuwa ni mbadala wa rakaa moja, basi idadi itakuwa ni shufa si witiri, na ikiwa kaswali rakaa nne kwa rakaa iliyozidi; basi atakuwa katekeleza wajibu wake pasina kuongeza wala kupunguza. Sijida mbili za kusahau zilikuwa ni kumdhalilisha Shetani na kumshinda, na kumrudisha akiwa kafedheheka, na kashindwa kufikia lengo lake; Kwa sababu alimvurugia swala yake, na akataka kuiharibu, na ikakamilika swala ya mwanadamu alipotekeleza amri ya Mwenyezi Mungu Mtukufu ya kusujudu, sijida ambayo Ibilisi aliasi, alipokataa kumtii Mwenyezi Mungu kwa kumsujudia Adamu.