explain-icon

Ufafanuzi

Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa sadaka haipunguzi mali, bali inaikinga na maafa, na Mwenyezi Mungu humpa badala mwenye nayo ya kheri kubwa, inakuwa ni ziada na sio kupungua. Na kusamehe kunapokuwa na uwezo wa kulipiza kisasi hakukuwahi kuzidisha kwa mwenye kusamehe isipokuwa nguvu na utukufu. Na hakuwahi kunyenyekea na kujidhalilisha yeyote kwa kutaka radhi za Allah, si kwa kumuogopa yeyote, na si kwa kujipendekeza kwa yeyote, na wala si kwa kutaka manufaa kwake, isipokuwa mtu huyu malipo yake yatakuwa ni kunyanyuliwa na kupewa utukufu.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kheri na kufaulu vinapatikana kwa kutekeleza sheria na kufanya mambo ya kheri hata kama baadhi ya watu watadhania kinyume na hivyo.