Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa atakayefunga mwezi wa Ramadhani kwa kumuamini Mwenyezi Mungu, na kwa kuitakidi ulazima wa swaumu na yale aliyoyaahidi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa wafungaji kuwa na malipo makubwa na thawabu, akikusudia kupata radhi za Allah Mtukufu si kwa kutaka kujionyesha au kusikika, yatasamehewa kwake madhambi yake yaliyopita.