Imesimuliwa kutoka kwa Sahal Mwenyezi Mungu amridhie, kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika Peponi kuna mlango unaoitwa Rayyani, watauingia wafungaji siku ya Kiyama, hato ingia ndani ya Pepo hiyo isipokuwa wafungaji, kutasemwa: Wapo wapi wafungaji? Watasimama hatoingia ndani yake isipokuwa wao, watakapoingia utafungwa kisha hatoingia ndani yake yeyote". Sahihi - Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake
explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kwamba mlango mmoja miongoni mwa milango ya Pepo unaitwa: Mlango wa Rayyan, wataingia hapo wafungaji siku ya Kiyama, hatoingia yeyote zaidi yao, patanadiwa: Wako wapi wafungaji, basi watasimama na wataingia, hatoingia hapo yeyote zaidi yao, atakapomaliza kuingia wa mwisho wao utafungwa, na hatoingia tena yeyote.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Amesema Nawawi: Katika hadithi hii kuna ubora wa swaumu na heshima kwa wafungaji.
  • Mwenyezi Mungu amewatengea wafungaji mlango katika milango minane ya Pepo, watakapouingia utafungwa.
  • Kumebainishwa kuwa Pepo inamilango.
  • Amesema Assanadi: Kauli yake: "Wako wapi wafungaji", yaani: Wenye kukithirisha kufunga, kama mtu muadilifu na dhalimu, husemwa kwa mtu aliyezoea hilo, na si kwa mwenye kufanya hilo mara moja.
  • "Rayyan" Yaani: Mwenye kukata kiu; kwa sababu wafungaji hupata kiu na hasa hasa katika siku za kiangazi zenye joto la muda mrefu; watalipwa kwa kuitwa mlango huu kwa kile kilichokuwa kinawahusu wao, mlango wa Rayyan, na imesemekana kuwa Rayyan ni wingi wa kulowesha koo kinyume cha kiu, na umeitwa hivyo; kwa sababu ndio malipo ya wafungaji kwa kiu yao na njaa yao.