explain-icon

Ufafanuzi

Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- Kuwa mwanadamu kamili katika kuunga udugu na kuwatendea wema ndugu wa karibu si yule mtu mwenye kulipa wema aliotendewa, Bali muunga udugu halisi na kamili katika kuunga udugu ni yule ambaye ukikatwa udugu wake anauunga, hata wakimtendea ubaya; basi yeye huwalipa wema.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kuunga udugu kunakozingatiwa kisheria ni kumuunga aliyekukata miongoni mwao, na kumsamehe aliyekudhulumu, na kumpa aliyekunyima, na si kuunga udugu kwa kubadilishana (wakiniunga nitawaunga wakikata nawakata) au kulipa wema uliotendewa.
  • Kuunga udugu kunakuwa kwa kufikisha kheri kwa kadiri ya uwezo, kwa kutumia mali na dua na kuamrishana mema na kukatazana maovu na mfano wake, na kuzuia yawezekanayo katika shari juu yao.