Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemuamrisha Muislamu kumsadia ndugu yake Muislamu sawa sawa awe kadhulumu au kadhulumiwa, mtu mmoja akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nimnusuru atakapokuwa emedhulumiwa kwa kumuondolea dhuluma, wasemaje ikiwa kadhulumu nitamsaidia vipi? Akasema: Utamzuia, na kumshika mkono na umkinge na umzuie na dhuluma; kwa kufanya hivyo ndiko kumnusuru dhidi ya Shetani wake na nafsi yake yenye kuamrisha maovu.