Ametubainishia sisi Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kuwa atakapotukataza kitu basi ni wajibu juu yetu kukiacha pasina kubagua, na atakapotuamrisha kwa chochote basi ni juu yetu kukifanya kile tunachokiweza. Kisha akatutahadharisha ili tusije kuwa kama baadhi ya umma zilizopita pindi walipokithirisha maswali juu ya Manabii wao ikiwa ni pamoja na kwenda kinyume nao, basi Mwenyezi Mungu akawaadhibu kwa aina mbali mbali za maangamivu na uharibifu, tunatakiwa tusiwe mfano wao ili tusiangamie kama walivyoangamia.