explain-icon

Ufafanuzi

Anakataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuyatelekeza majumba kwa kutoka swali ndani yake, yakawa kama makaburi yasiyoswaliwa ndani yake. Kisha akaeleza -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa Shetani hukimbia nyumba ambayo husomwa suratul Baqara ndani yake.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kumependekezwa kuzidisha ibada na swala za sunna ndani ya majumba.
  • Haifai kuswali makaburini; kwa sababu ni njia katika njia za shirki na kuwakweza wafu, isipokuwa swala ya jeneza.
  • Katazo la kuswali makaburini limethibiti kwa Masahaba, na kwa sababu hiyo amekataza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- nyumba kufanywa mfano wa makaburi hakuswaliwi ndani yake.