Alipoteremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Mtume wake rehema na amani ziwe juu yake kauli yake: "Ni vya Mwenyezi Mungu vilivyoko mbinguni na Ardhini" Kwa kuviumba na kuvimiliki, na maamuzi na kuvipangilia, "Na ikiwa mtadhihirisha" na mkaonyesha wazi na mkatangaza "yaliko ndani ya nafsi zenu" na vifua vyenu "au mkayaficha" mkayasitiri na kuyaficha ndani ya nyoyo zenu "atakuhesabuni Mwenyezi Mungu" siku Kiyama. "basi anamsamehe amtakaye" kwa fadhila zake na rehema zake, "na anamuadhibu amtakaye" kwa uadilifu wake, "na Mwenyezi Mungu juu ya kila kitu ni muweza" hakimshindi chochote. Maswahaba walipolisikia hilo liliwapa uzito sana; kwa sababu ndani yake kuna kuadhibiwa mpaka kwa yale yaliyoko moyoni, miongoni mwa fikira. Wakamjia Mtume rehema na amani ziwe juu yake, kisha wakashuka chini kwa kupiga magoti, wakasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, tumepewa majukumu kabla ya hili miongoni mwa amali za mwili yale tuwezayo kuyafanya; mfano kama swala na swaumu na Jihadi na sadaka, lakini imeteremshwa kwako aya hii na wala hilo hatuliwezi. Akasema kuwaambia rehema na amani ziwe juu yake: Hivi mnataka kusema kama walivyosema Mayahudi na Wakristo: "Tumesikia na tumeasi"? bali semeni: "Tumesikia na tumetii, tunataraji msamaha kutoka kwako Mola wetu, na marejeo ni kwako", Maswahaba kuitika amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, wakasema: Tumesikia na tumetii, tunataraji msamaha kutoka kwako Mola wetu, na marejeo ni kwako. Walipolizungumza hilo Waislamu kwa ndimi zao, na nyoyo zao zikatii; Mwenyezi Mungu akateremsha sifa njema kwa Mtume na Umma wake kwa kauli yake: "Ameamini Mtume yale yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake na waumini (pia wameamini hivyo)" na zikanyenyekea ndimi zao na nyoyo zao kwa amri ya Mwenyezi Mungu. "Wote wamemuamini Mwenyezi Mungu na Malaika wake na vitabu vyake na Mitume wake, hatutofautishi yeyote katika Mitume wake". Bali tunawaamini wote "na wakasema tumesikia" kauli yako "na tumetii" amri yako, na tunaomba "maghufira yako Mola wetu" na msamaha wako, "na marejeo ni kwao" na mafikio siku itakaposimama hesabu, walipofanya hivyo, na wakasema walichoamrishwa kusema kama kudhihirisha usikivu na utiifu kwa amri za Mwenyezi Mungu; akaupunguzia Mwenyezi Mungu Umma huu na akaifuta aya hiyo, kwa kauli yake: "Hailazimishi Mwenyezi Mungu Nafsi ila kwa kadiri ya wasaa wake" na uwezo wake na nguvu zake na juhudi zake, "ina" thawabu "za yale iliyoyachuma" na kuyafanya miongoni mwa kheri, "na inabeba" adhabu "za yale iliyoyachuma" kama mzigo wa dhambi, na hamuadhibu Mwenyezi Mungu kwa dhambi la mtu mwingine, wala kwa yale yaliyotiwa wasi wasi na nafsi yake. "Mola wetu, usituadhibu" na ukatutesa "ikiwa tutasahau" tukawa hatukukumbuka, "au tukakosea" tukaiacha haki si kwa makusudi, Mwenyezi Mungu akawajibu kwa hilo akasema: Ndiyo, nimefanya hivyo. "Mola wetu Mlezi usitubebeshe mazito" na mashaka na magumu "kama ulivyowabebesha wale waliokuwa kabla yetu" katika wana wa Waisraeli na wengineo, Mwenyezi Mungu akapokea na akasema: Ndiyo, nimefanya hivyo. "Mola wetu Mlezi na wala usitubebeshe tusiyoyaweza" miongoni mwa majukumu na mabalaa na mambo ambayo hatuwezi kuyabeba, akasema Mwenyezi Mungu: Ndiyo nimefanya hivyo, "na utusamehe" madhambi yetu na utufutie, "na utughufirie" madhambi yetu na uyasitiri, "na uturehemu" kwa rehema zako pana, "wewe ndiye Mole wetu" na bwana yetu; "tunusuru" kwa kusimamisha hoja na ushindi "kwa watu makafiri" katika kupigana nao na kupambana nao, Mwenyezi Mungu akapokea, akasema kuwaambia: Naam, nimefanya hivyo.