explain-icon

Ufafanuzi

Ameeleza Ukba bin Aamiri radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alisema kumwambia: Usiku huu Mwenyezi Mungu kaniteremshia aya, hazijawahi kuonekana mfano wake katu -yaani katika kuomba kinga- nazo ni sura mbili za kinga: Suratu (Qul Auudhubirabbil falaq), na suratu (Qul Auudhubirabbin naas).

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Kumebainishwa ukubwa wa fadhila wa sura mbili hizi.
  • Himizo la kuomba kinga kupitia sura hizi dhidi ya kila shari.