Alimuijia kiongozi wa waumini Ally bin Abii Twalib radhi za Allah ziwe juu yake bwana mmoja mtumwa alikuwa kaandikishana na bwana yake na amekubaliana naye ili aikomboe nafsi yake na aiache huru ili awe huru, na hakuwa na mali, akasema: Hakika mimi nimeshindwa kulipa deni hilo juu yangu, nakuomba unisaidie kulilipa kwa mali, au kwa kunifundisha na kunielekeza, akasema kumwambia kiongozi wa waumini: Je, nikufundishe maneno aliyonifundisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake, lau kama ungelikuwa na deni mfano wa mlima Swiri wa kabila la Twayyi basi Mwenyezi Mungu angelikulipia kwa mstahiki wake, na angelikuokoa kutoka katika madhila yake, akasema: Sema: "Ewe Mwenyezi Mungu nitosheleze" na uniepushe na uniweke mbali "kwa halali yako" nitosheke nayo "dhidi ya" kutumbukia katika "haramu yako", na unitosheleze "kwa fadhila zako" na ukarimu wako "kutomuhitaji yeyote" katika viumbe.