Ameeleza Hudhaifa radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba wanapohudhuria chakula pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake hawaweki mikoni yao katika chakula mpaka kwanza aanze Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuweka mkono wake, na hakika sisi tulihudhuria pamoja naye siku moja katika chakula, akaja kijakazi mmoja, kutokana na kasi yake kana kwamba anasukumwa, akaenda ili aweke mkono wake katika chakula, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akamshika mkono wake, kisha akaja Bedui kana kwamba anasukubwa, akamshika mkono wake kabla hajagusa chakula, akasema Mtume rehema na amani ziwe juu yake: Hakika Shetani hupata uwezo wa kula chakula, atakapoanza mtu kula chakula pasina kumtaja Mwenyezi Mungu Mtukufu, na alikuja na kijakazi huyu ili ajihalalishie kula, nikamshika mkono wake, kisha akaja na huyu Bedui, ili akihalalishe nikamshika mkono wake, ninamuapa yule ambaye nafsi yangu iko mkononi mwake, hakika mkono wa Shetani ulikuwa mkononi mwangu pamoja na mkono wake, kisha akataja jina la Mwenyezi Mungu Mtukufu na akala.