explain-icon

Ufafanuzi

Alikuwa rehema na amani ziwe juu yake anapopiga chafya: Jambo la kwanza: Anaweka mkono wake, au nguo yake juu ya kinywa chake; Kisije kutoka kinywani mwake au puani mwake chochote kitakachomuudhi aliyekaa naye. Jambo la pili: Anashusha sauti yake na wala hainyanyui.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Hapa pamebainishwa muongozo wake rehema na amani ziwe juu yake, ikiwa ni pamoja na kumuiga katika hilo.
  • Inapendekeza kuweka nguo au leso au mfano wa hayo mdomoni na puani mtu anapopiga chafya, ili kitu chochote kisitoke humo kitakachomuudhi mtu aliyekaa naye.
  • Kupunguza sauti ya mtu wakati wa kupiga chafya kunahitajika, na ni ishara ya adabu kamili na maadili mema.