Anabainisha Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- yakuwa mja mwenye kumuamini Mwenyezi Mungu na siku ya mwisho ambayo ndani yake kuna marejeo yake na malipo ya matendo yake, basi imani yake inamuhimiza kufanya mambo haya. La kwanza: Kauli njema: Kama tasbihi (kusema: Sub-haanallah) na tahlili (Laa ilaaha illa llaah) na kuamrisha mema, na kukataza mabaya, na kuwasuluhisha watu, ikiwa hatofanya hivyo basi ashikamane na ukimya, na ajizuie na maudhi yake, na ahifadhi ulimi wake. La pili: Kumkirimu jirani: Kwa kumtendea wema na kutomuudhi. La tatu: Kumkirimu mgeni anayekuja kukutembelea: Kwa maneno mazuri na kumlisha chakula na mfano wa hayo.