Amehimiza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- juu ya kutenda wema, na mtu asiudharau hata kama utakuwa kidogo, na miongoni mwake ni ukunjufu wa uso kwa kutabasamu wakati wa kukutana, ni lazima kwa muislamu alipupie hilo; kwa sababu hujenga kuwa na ukaribu na ndugu yako muislamu na huingiza furaha kwake.