Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake namna ya biashara sahihi katika aina sita za riba, nazo ni: Dhahabu, fedha, ngano (ambayo haijakobolewa), na ngano (iliyokobolewa), na tende, na chumvi, ikiwa ni katika aina hiyo hiyo, kama kuuza dhahabu kwa dhahabu na fedha kwa fedha....ni lazima kuwe na sharti mbili: Ya kwanza: Kufanana katika uzito ikiwa ni kitu kinachopimika kama dhahabu na fedha, au kufanana katika kipimo ikiwa ni kitu kinachopimika, kama ngano (ambayo haijakobolewa) na ngano (iliyokobolewa) na tende na chumvi. Ya pili: Ni muuzaji kupokea thamani na mnunuzi kupokea bidhaa, na hilo lifanyike katika kikao cha makubaliano ya biashara. Zikitofautiana aina zote hizi kama kuuza dhahabu kwa fedha, na tende kwa ngano kwa mfano, itafaa kuuza kwa sharti moja, nayo ni muuzaji kupokea thamani na mnunuzi kupokea bidhaa katika kikao cha makubaliano, isipofanyika hivyo biashara itakuwa batili, na muuzaji na mnunuzi watakuwa wameingia ndani ya riba katika hilo wote wawili.