Amebainisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa atakapotawadha muislamu au muumini akaosha uso wake wakati wa udhu, yanatoka katika uso wake makosa yote madogo madogo aliyoyatazama kwa macho yake pamoja na maji ya yanayodondoka baada ya kuosha, au pamoja na tone la mwisho la maji, akiosha mikono yake yanatoka katika mikono yake makosa yote madogo madogo iliyoyachuma mikono yake au pamoja na tone la mwisho la maji, na akiosha miguu yake yanatoka makosa yake yote madogo madogo iliyotembea kuyafuata miguu yake, mpaka atoke akiwa kasafishika na madhambi madogo madogo kwa kumalizika kwa udhu.