Anaeleza Mtume -Rehema na amani ziwe juu yake- kuwa mwenye kusimamia masilahi ya mwanamke aliyefiwa na mumewe na ikawa hakuna yeyote mwenye kusimamia mambo yake, na masikini muhitaji, na akawapa matumizi akitaraji malipo mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, basi mtu huyu katika malipo ni kama mpigana Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu, na ni kama mwenye kusimama katika swala ya tahajudi asiyechoka, na mfungaji asiyefungua.