Walikuja watu wawili kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika Hija ya kuaga, wakati akigawa sadaka, na wakamuomba awapatie katika sadaka hizo, Mtume rehema na amani ziwe juu yake akawa anawatazama mara kwa mara, ili ajue hali zao, na je, ni halali kwao kupewa sadaka au la? Akawaona ni wanaume wawili wenye nguvu, akasema: Ikiwa mtapenda nitawapa katika sadaka hizi, lakini hana fungu ndani yake mwenye mali inayomtosheleza, wala kwa mwenye uwezo wa kutafuta na kuchuma mali, hata asipokuwa na mali inayomfanya ahesabike miongoni mwa wenye uwezo.