Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kutoa kiapo kwa Mwenyezi Mungu huku muapaji akijua kuwa anaapia uongo ndani yake, ili ajipatie kwa kiapo hiki mali ya mwenzake; huyu atakutana na Mwenyezi Mungu akiwa kamkasirikia, akaeleza Ash'athi bin Kaisi radhi za Allah ziwe juu yake ya kuwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake alilisema hilo wakati ambao kulikuwa na mzozo kati yake yeye na bwana mmoja Yahudi katika umiliki wa Ardhi, wakashitakiana kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake, akasema kumwambia Ash'athi: Unatakiwa kuleta ushahidi ili kuthibitisha madai yako, ukishindwa kuuleta basi hutokuwa na haki zaidi ya kiapo cha hasimu wako mshitakiwa, Ash'athi akasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, basi huyu bwana Yahudi si ataapa pasina hofu na mali yangu itapotea, akateremsha Mwenyezi Mungu Mtukufu kusadikisha hilo ndani ya Qur'ani kauli yake Mtukufu: "Hakika wale wanaouza" na wanabadilisha "ahadi ya Mwenyezi Mungu", na usia wake kwa waumini kwa kutimiza amana "na viapo vyao" na viapo vyao kwa jina lake kwa uongo "kwa thamani ndogo" kwa starehe za dunia "Hao hawana fungu lolote kwao Akhera" wala sehemu "Wala hatowasemesha Mwenyezi Mungu", kwa maneno yanayowafurahisha na kuwanufaisha, bali atawaghadhibikia, "wala hatowatazama siku ya Kiyama", mtazamo wa huruma na wema, "wala hatowatakasa" kwa kuwasifia kwa mazuri, wala hatowasafisha kwa kuwapa msamaha wa madhambi na machafu "na watakuwa na adhabu chungu" yenye kuumiza kwa sababu ya yale waliyoyafanya.