Aliulizwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu matendo yanayopelekea kuingia Peponi au kuhusu matendo yanayopendwa zaidi na Mwenyezi Mungu? Basi rehema na amani za Allah ziwe juu yake akamwambia muulizaji: Dumu na sijida kwa wingi, kwani kila unapomsujudia Mwenyezi Mungu anakunyanyua daraja kwayo, na anakusamehe dhambi kwa sababu ya sijida hiyo.