explain-icon

Ufafanuzi

Ameamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha lile linalokutia shaka ndani yake katika kauli na matendo kuwa limekatazwa au la, je ni halali au ni haramu, na ufanye yale usiyo na shaka nayo katika yale uliyo na uhakika na uzuri wake na uhalali wake.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Muislamu anatakiwa kujenga mambo yake juu ya yakini na kuacha yenye kutia shaka ndani yake, na awe na utambuzi katika dini yake.
  • Katazo la kutumbukia katika matamanio mabaya.
  • Ukitaka utulivu na raha achana na mambo yanayokutia shaka na kuyatupilia mbali.
  • Huruma ya Mwenyezi Mungu kwa waja wake, pale alipowaamrisha katika mambo ambayo ndani yake kuna raha ya moyo, na akawakataza katika yale yanayotia msongo na utata.