Aliamrisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuacha kile ulicho na shaka nacho katika maneno na matendo nakuwa jambo hilo limekatazwa toka mwanzo, je jambo hili ni halali au ni haramu, afanye asilo na shaka nalo katika yale ambayo anaamini kuwa ni mazuri na ni halali, kwa sababu moyo unatulizana na unatulia katika hilo, na hakuna shaka ndani yake inayotia msongo na taharuki.