Aliulizwa mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake kuhusu tabia za Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema: Haikuwa katika tabia zake uchafu na ubaya wa kauli na vitendo, na wala hakuwa akijilazimisha machafu wala kuyakusudia, wala hakuwa mpiga kelele kwa kunyanyua sauti yake masokoni, na wala alikuwa halipi ubaya kwa ubaya; lakini alikuwa akilipa ubaya kwa wema, na akisamehe ndani ya moyo, na akifuta kosa na kulipuuza katika dhahiri.