Alieleza Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuhusu neema mbili kubwa miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu kuwa wanapata hasara ndani yake watu wengi, kiasi kwamba wanazitumia mahali pasipostahiki; kwani mwanadamu zikikusanyika kwake neema ya afya na wakati, akazidiwa na uvivu wa kufanya ibada basi kapata hasara; na ndio hali ya watu wengi, na akiutumia muda wake na afya yake katika kumtii Mwenyezi Mungu basi atakuwa kapata faida; hii ni kwa sababu dunia ndio shamba la Akhera, na wakati hufuatiwa na shughuli, na afya hufuatiwa na maradhi, na lau kusingekuwa na chochote zaidi ya uzee basi ungetosha.