Mtume rehema na amani ziwe juu yake amemuamrisha muislamu kumtazama katika mambo ya dunia katika nafasi na mali na cheo na mengineyo yule ambaye ana hali ya chini zaidi, na asimtazame katika mambo ya dunia yake yule aliyeko juu yake na bora zaidi kuliko yeye, kwa kumtazama aliyeko chini ni bora na kunastahiki zaidi kumfanya asidharau na kuzidogesha neema za Mwenyezi Mungu zilizo juu yake.