Imepokelewa kutoka kwa Abii Saidi Al-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake amesema: "Hakika ndani ya Pepo kuna mti ambao anatembea aliyepanda kipando madhubuti chenye uimara na kasi kubwa ya kukimbia kwa muda wa miaka mia moja na haumalizi (kuuvuka) mti huo". Sahihi - Wamekubaliana Bukhari na Muslim juu ya usahihi wake