Walitajwa watu wawili kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake mmoja wao ni mchamungu, na mwingine msomi, ni yupo mbora kati yao? Akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ubora wa msomi wa elimu ya kisheria mwenye kuifanyia kazi na mwenye kuifundisha kwa mchamungu aliyejitenga kwa ajili ya ibada, pamoja na kujua kwake yale ya wajibu kwake katika elimu ni kama ubora wake rehema na amani ziwe juu yake na utukufu wake kwa Swahaba wa chini zaidi. Kisha akabainisha rehema na amani ziwe juu yake sababu ya hilo, kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu, na Malaika wake miongoni mwa wabeba Arshi, na wakazi wa mbinguni katika Malaika wengineo, na wakazi wa Ardhi kwanzia binadam na majini na wanyama wote, hata mdudu chungu katika makazi yake ndani ya tumbo la Ardhi, na hata nyangumi na samaki wa Baharini; alitaja hivi ili waingie katika kauli hii viumbe wa nchi kavu na Baharini, wote hawa wanamuombea mazuri mwenye kuwafundisha watu elimu ya dini ambayo ndani yake kuna uokovu wa watu na mafanikio yao.