explain-icon

Ufafanuzi

Maana ya hadithi: Nikuwa atakayetoka nyumbani kwake au katika mji wake; kwaajili ya kutafuta elimu ya kisheria,huyo anakuwa katika hukumu ya aliyetoka kwaajili ya Jihadi katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu,mpaka atakaporudi kwa watu wake; kwasababu anakuwa ni kama mpiganaji katika kuihuisha kwake dini na kumdhalilisha shetani na kuitaabisha nafsi.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Nikuwa kutafuta elimu ni kupambana katika njia ya Mwenyezi Mungu.
  • Mwenye kutafuta elimu ana malipo ya mpiganaji katika viwanja vya mapambano; kwasababu wote hao wanayasimamia yale yanayoweza kuipa nguvu sheria ya Mwenyezi Mungu na wanazuia yasiyokuwa humo.
  • Ndani yake nikuwa mwenye kutoka katika kutafuta elimu atakuwa na malipo ya kutembea kwake na kwenda kwake na kurudi kwake mpaka atakaporejea kwa watu wake.