Mtu mmoja alilalamika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake kuwa ana ndugu wa karibu wa ukoo anaamiliana nao kwa wema ila wao wanaamiliana naye kinyume na hivyo; anawaunga na kuwatembelea ila wao wanamtenga, na anawatendea ihisani kwa wema na uadilifu ila wao wanamtendea ubaya kwa ujeuri na ukaidi, na anakuwa mpole kwao na kuwasamehe ila wao wanampuuza kwa kumfanyia mabaya katika kauli na vitendo, je, aendelee kuwaunga udugu pamoja na hayo yote yaliyotajwa? Mtume rehema na amani ziwe juu yake akasema kumwambia: Ikiwa ni hivyo kama ulivyoeleza basi wewe unawafedhehesha na kuwadharaulisha katika nafsi zao, ni kana kwamba unawalisha majivu ya moto; kwa wingi wa wema wako na kwa ubaya wa matendo yao mbele ya nafsi zao, na bado anaendelea kuwa pamoja nawe msaidizi kutoka kwa Mwenyezi Mungu dhidi yao, na wao waendelee katika kukutendea ubaya.