Ameeleza mama wa waumini Aisha radhi za Allah ziwe juu yake yakwamba Mtume rehema na amani ziwe juu yake alidumu na itikafu katika siku kumi za mwisho wa Ramadhani, kwa ajili ya kuutafuta usiku wenye cheo (Lailatul-Qadri), na akaendelea katika hilo mpaka Mwenyezi Mungu alipomfisha, na wakadumu na itikafu wake zake baada yake, radhi za Allah ziwe juu yao.