Ameeleza Abdallah bin Masudi radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba wao walikuwa pamoja na Mtume rehema na amani ziwe juu yake katika safari, akaondoka rehema na amani ziwe juu yake kwa ajili kukidhi haja yake, Maswahaba zake wakapata ndege aina ya Hummara akiwa na makinda mawili, wakayachukua, yule ndege akaanza kupeperusha mbawa zake na kuzipepesa kwa huzuni kwa kuwakosa makinda wake, akaja rehema na amani ziwe juu yake na akasema: Ni nani aliyemuhuzunisha na akamuhofisha kwa kuchukua vitoto vyake? Kisha akaamrisha virejeshwe kwake. Kisha akaona kijiji cha wadudu chungu kilichochomwa kwa moto, akasema rehema na amani ziwe juu yake: Ni nani aliyekiunguza hiki? Wakasema baadhi ya Maswahaba: Sisi. Akasema kuwaambia: Hakika haifai kwa yeyote kuadhibu kiumbe hai kwa moto; isipokuwa Mwenyezi Mungu muumba wake.