explain-icon

Ufafanuzi

Mtume rehema na amani ziwe juu yake aliona mwanamke akiwa kauwawa katika moja ya vita, akakemea vikali kuuwawa wanawake na watoto ambao hawajafikia balehe.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Mwanamke na mtoto yeyote ambaye hatopigana, na mwenyekuwa mfano wao kama wazee vikongwe, na watawa, hawa hawauawi, madam hawajatoa rai au msaada wowote wa kuwapiga waislamu, ikiwa watafanya hivyo basi nao watauawa.
  • Katazo la kuwaua wanawake na watoto; kwa sababu hawa huwa hawawapigi vita waislamu, na malengo ya kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, ni kuvunja nguvu ya wapiganaji pekee, ili ujumbe wa haki uwafikie watu wote.
  • Huruma ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake mpaka katika mapambano na vita.