Ameeleza Laqitwu bin Swabira radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake ya kwamba yeye alifika kwa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwa pamoja na watu wengine kutoka katika jamii yake ya Bani Muntafiq, anasema: Hatukumkuta nyumbani kwake, na tukamkuta Mama wa Waumini Aisha radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake, akaamrisha tuandaliwe mkate wa ngano na samli, na tukaletewa bakuli la tende. Kisha akaja rehema na amani ziwe juu yake, akasema: Je, mmeletewa chochote katika chakula? Tukasema: Ndiyo, anasema Laqitwu: Wakati tukiwa bado tumekaa naye rehema na amani ziwe juu yake, ghafla akaja mchungaji wa mbuzi wa Mtume rehema na amani ziwe juu yake akiwaswaga kwenda katika zizi lake, huku akiwa kabeba kitoto cha mbuzi kikipiga kelele, akasema: Umezalisha nini? Akasema: Jike. Akasema: Basi tuchinjie badala yake mbuzi mwingine mkubwa, kisha akasema rehema na amani ziwe juu yake: Usidhanie kuwa sisi kwa ajili yenu tumejikalifisha na tukamchinja, bali sisi tuna mbuzi idadi yake ni mia moja, na wala hatutaki wazidi katika idadi hii, akizaliwa mbuzi mpya tunachinja badala yake mbuzi mwingine, akasema Laqitwu: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hakika mke wangu ulimi wake ni mrefu na ana maneno machafu, nifanye nini kwake? Akasema: Basi mpe talaka. Anasema: Nikasema: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakika nimeishi naye muda mrefu sana, na nimezaa naye. Akasema: Basi mpe nasaha, ikiwa ndani ya moyo wake kutakuwa na kheri atazifanyia kazi nasaha zako, na ikiwa hatobadilika, basi mpige kipigo kisichojeruhi, na wala usimpige kama unavyompiga mtumwa wako. Kisha akasema Laqitwu: Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nieleze kuhusu Udhu. Akasema: Fikisha maji ya Udhu mahala pake, na ukipe kila kiungo haki yake, na wala usiache kitu katika faradhi zake na sunna zake, na achanisha vidole vya mikono yako na miguu yako wakati wa kuviosha, na upitilize katika kuyavuta maji ndani ya pua yako wakati wa udhu na kuyatoa kwake, isipokuwa ikiwa ulitia nia ya swaumu ili maji yasiingie tumboni mwako.