explain-icon

Ufafanuzi

Alichukua Mtume rehema na amani ziwe juu yake nguo ya hariri au kipande chake, kwa mkono wake wa kushoto, na akachukua pambo la dhahabu au mfano wake kwa mkono wake wa kulia, kisha akasema: Hakika hariri na dhahabu ni haramu kuvivaa kwa wanaume, ama wanawake hivyo ni halali kwao.

explain-icon

Katika Faida za Hadithi

  • Amesema As- Sanadi: (Haram): Makusudio yake ni kuvitumia kwa kuvaa; na matumizi mengine ni ruhusa kwa wote, kama kubadilishana, kuvitoa sadaka na kuuza, na kutumia dhahabu kwa kufanya vyombo na kuvitumia ni haramu kwa wote.
  • Sheria ya Uislamu imepanua wigo kwa wanawake kwakuwa wao wanahitaji zaidi mapambo na mfano wake.