Dua ya Mtume rehema na amani ziwe juu yake ya kulaaniwa na kufukuzwa na kuwekwa mbali na rehema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa makundi ya aina nne: La kwanza: Mwanamke mwenye kuunga nywele zake au za mwenzake kwa nywele zingine. La pili: Na mwenye kutaka kuungwa nywele, kwa kumuomba mwenzake amuunganishe nywele zake kwa nywele zingine. La tatu: Mwenye kupiga chata, na anayejichoma sindano katika sehemu ya mwili wake, kama uso au kiganja au kifua, na kuweka wanja au mfano wake, ili kubakie alama ya bluu, au kijani; kwa kutaka kujipamba au uzuri. La nne: Mwenye kutaka kupigwa chata, ni yule anayeomba kupigwa chata. Na matendo haya ni katika madhambi makubwa.