Ametahadharisha Mtume rehema na amani ziwe juu yake kushusha chini zaidi ya miguu kila kinachositiri kuanzia chini ya mwili wake kama nguo au suruali au kinginecho, na kinachokuwa zaidi ya kongo mbili katika miguu miongoni mwa kikoi kinachoburuza basi hicho ni motoni ikiwa ni adhabu kwake kwa kitendo hicho.